Salome ni filamu ambayo nimeitunga kutokana na nyimbo yangu ya Salome. Ila filamu hii bado ipo kwenye maandishi na haijachezwa. Kwa sasa tunatafuta mfadhili ili aweze kuwekeza katika filamu hii ili iweze kuchezwa kwa vitendo.
Kama umevutiwa na story na unapenda kunisapoti bonyeza hapo na tafuta mawasiliano na mimi.
Hapo chini unasoma story ya Salome:
SALOME
FILM 2012
SALOME
Wasifu wake
§ Awe msichana mwenye umri wa miaka 16
§ Awe na rangi ya maji ya kunde
§ Umbo sio mnene wala sio mwembamba
§ Asiwe mrefu wala mfupi, mpole, mcheshi. Ni mwanafunzi wa shule ya msingi darasa la saba anapenda sana kusoma na kushirikiana na wenzake katika mambo mbalimbali.
MAMA SALOME
Wasifu wake
§ Awe mtu mzima mwenye umri wa miaka 35
§ Rangi ya maji ya kunde
§ Asiwe mrefu wala mfupi
§ Awe mnene kiasi
§ Anapenda kazi za nyumbani na kusuka ukili
§ Mcheshi mwenye maneno mengi
§ Anapenda utamaduni
BABA SALOME
Wasifu wake
§ Awe mtu mzima mwenye umri wa miaka 37
§ Mrefu kiasi na mwembamba kiasi
§ Mweusi kidogo
§ Awe mkali anachokiongea
§ Anapenda kifanyiwe kazi
§ Anapenda kukaa nyumbani
BABU SALOME
Wasifu wake
§ Awe mwenye miaka 60
§ Mrefu kiasi na mwembamba kiasi
§ Mweusi kidogo
§ Awe mcheshi anapenda matani
§ Anapenda sana utamaduni
§ Anapenda kukaa na panga muda wote
BIBI SALOME
Wasifu wake
§ Awe mwenye umri wa miaka 54 hadi 57
§ Mfupi kiasi
§ Rangi yake ni maji ya kunde
§ Awe mpenda kukubali kila jambo
§ Awe anayependa kutembea peku
§ Anapenda kulima
§ Awe mwembamba kidogo
SINI: 1
Salome anaonekana darasani akiwa na wenzake huku mwalimu akiwa ana fundisha na Salome akionekana akiwa mwepesi wa kujibu maswali ya somo la Kiswahili.
MWALIMU
Mwalimu anandika ubaoni kisha anawageukia wanafunzi na kuwauliza maswali.
Mgaagaa na upwa?
SALOME
Anasimama na kujibu swali.
Hali wali mkavu.
MWALIMU
Anaonekana akimsifia Salome alivyojibu vizuri.
Safi sana Salome mpigieni makofi.
WANAFUNZI WOTE
Wakipiga makofi wengine wakipiga juu ya dawati.
MWALIMU
Mwalimu anaoneka akiwapa maelezo wanafunzi kuhusu mtihani wa kumaliza darasa la saba akiwapa moyo wanafunzi kuhusu swala lakujisomea wakiwa nyumbani.
KATI KUBWA
Wanafunzi wanaonekana wakitawanyika kuelekea majumba. Salome anaonekana akikimbia nyumbani kwao.
SINI: 2
NYUMBANI KWA KINA SALOME (MCHANA)
Mama Salome anapepea moto wa kuni. Sufuria ya mihogo ikiwa juu ya majifya. Baba Salome akiwa kakaa uwanjani kwenye kiti mara anamuita Mama Salome.
BABA SALOME
Akimuangalia usoni na tabasamu.
Unajua nini, Mama Salome kesho jumamaosi Salome haendi shule, uwahi kumwamsha mapema ili awahi shamba.
MAMA SALOME
Akimwangalia Baba Salome kwa uwoga na mshangao.
Lakini kesho wanaendaga kwajili ya mtihani wa kila wiki na hata hivyo uwa haendi bila 200 ili afanye mtihani wa wiki inaweza ikamsaidia siku ya mtihani wa mwisho.
BABA SALOME
Akimwangalia kwa hasira
Sina hiyo hela na nimesema kesho aende shamba.
MAMA SALOME
Akiwa na uwoga.
Lakini mume wa…
BABA SALOME
Naomba ukaendelee na kazi.
MAMA SALOME
Mama Salome ananyanyuka na kuelekea jikoni.
SINI: 3
Asubuhi
Salome na mama yake wakiwa shambani wanalima mara Mama Salome anaacha jembe na kukaa chini.
SALOME
Akimfuata Mama yake akiwa kashika jembe na kukaa chini.
Vipi? Mama?
MAMA SALOME
Akiguna huku akimwangalia Salome
Mmh! Nimechoka tu.
SALOME
Akitabasamu
Basi tuondoke.
MAMA SALOME
Anachukua jembe lake.
Haya twende, maana ninavyo jisikia.
WOTE
Mama Salome na Salome wanaonekana wakiweka jembe begani na kuondoka. Wakiwa njiani Salome anamsimulia mama yake mitihani ya shuleni kwao inayotolewa.
SALOME
Mama tumebakisha miezi mitatu tufanye mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.
MAMA SALOME
Sawa lakini umejiandaa vizuri na mtihani?
SALOME
Akishusha jembe begani na kulishika mkononi, huku akimwangalia mama yake.
Sina uhakiaka sababu mtihani ule wakujipima nilikuwa mtu wa pili kati ya watoto thelathini.
MAMA SALOME
Akimwangalia Salome.
Sawa umesema mtihani uliopita, lakini huu kila mtu anakuwa anajiandaa sana.
SALOME
Akimwangalia kwa kuhuzunika mama yake.
Mama niamini!
MAMA SALOME
Haya, na kusisitiza tu kwa sababu uliniambia unataka kuwa daktari.
WOTE
Wanaangaliana na kucheka.
KATI KUBWA
Wasichana watatu rafiki zake Salome wakiwa kisimani wanafua.
RAFIKI NO: 1 MARIAMU
Akimuomba Jeni sabuni akinyoosha mkono.
Jeni, niazime sabuni yako kidogo yangu imeisha.
JENI
Akibinua mdomo kwa dharau.
Ehe, mwenzangu mama kaniambia nisiimalize. Siwezi kukupa!
MARIAMU
Akiachia mdomo kwa mshangao.
Kwani nimekuambia namaliza si kidogo tu.
JENI
Akiendelea kufikicha nguo iliyokuwa kwenye ndoo.
Kwa kifupi sitaki wewe umezoea kumuomba Salome leo sasa hayupo na mimi sitaki.
RAFIKI NO: 3 HAPPY
Akibinua mdomo na kuguna.
Jeni tabia mbaya kwani mama yako atajua. Loo!
JENI
Akimwangalia Happy.
Haya, kuhusu wewe simpe.
HAPPY
Akichukua sabuni yake.
Ndio nampa.
Akimpa sabuni Mariamu.
MALIAMU
Akipokea huku, akitasamu.
Asante Happy. Lakini Jeni utakuwa na shida tu! Tutaonana.
JENI
Akiinuka akashika nguo na kwenda kuwanika.
Kwani sasa hivi sikuoni?
SINI : 4
USIKU
Salome anaonekana kakaa chumbani kwake kitandani akijisomea huku kibatari kikiwaka baada ya muda anazima kibatari anaamua kulala huku akijifunika kanga.
SINI:5
ASUBUHI: SHULENI
Wanafunzi wote wapo darasani pamoja na Salome. Wanafunzi wengine wanajisomea. Salome na rafiki zake watatu wanaongea kuhusu mtihani. Mara mwalimu anaingia darasani na kunyamazisha kelele. Mara anamuita Salome atoke mbele ya darasa.
MWALIMU
Hivi wewe Salome baada ya kusoma umekaa unawasimulia wenzio. Sijui stori gani hivi una akili wewe.
SALOME
Akimwangalia mwalimu usoni.
Hapana mwalimu nilikuwa naongea kuhusu mtihani wa taifa ili tujiandae sana.
MWALIMU
Akimtolea macho Salome na kukunja sura.
Muongo mkubwa kwanza, angalia hizo uniform zako zilivyo chanika!
SALOME
Akijiangalia.
Lakini mwalimu…
MWALIMU
Akiongea kwa sauti yenye hasira.
Kelele! Sasa uwende kwenu mpaka uje na uniform mpya.
SALOME
Kwa huzuni anatoka nje huku akiwaangalia wanafunzi wenzake.
WANAFUNZI
Wengine wakimwangalia Salome kwa huruma na wengine wanaendelea kusoma madaftari yao.
KATI KUBWA
Salome anaonekana amekaa na wazazi wake mbele ya nyumba yao (uwanjani). Baba akiwa kakaa kwenye kiti huku akishika fimbo. Na Salome na mama yake wamekaa kwenye mkeka. Salome anawaambia wazazi wake kilichomfanya arudi nyumbani mapema.
MAMA SALOME
Akimwangalia baba Salome usoni.
Kwani sisi masikini tukiwa hatuna hela ya kununua uniform ina maana mtoto hasomi? Basi makubwa!
BABA SALOME
Akipigisha chini fimbo yake huku akoingea.
Hivi nyinyi hamjui maskini ni maskini. Akipata bahati kidogo vikwazo vingi vitatokea sasa yote ya nini?
MAMA SALOME
Akiguna kwa mshangaoa.
Unamaanisha nini kusema hivyo?
BABA SALOME
Akimwangalia Salome.
We Salome hebu nenda kabadillishe nguo, ukae tu. Ikifika siku ya kuolewa uwolewe hakuna kingine.
MAMA SALOME
Akimtolea macho baba Salome.
Sasa hayo ndio maneno gani? Badala ya kuwaza tufanyaje ili mtoto aendelee na shule.
BABA SALOME
Akinyanyuka na kuelekea shambani.
Waza wewe utatafanyaje. Mimi naenda shamba kuangalia ndege.
MAMA SALOME
Akiguna na kunyanyuka kuelekea ndani.
Makubwa basi!
SINI:6
Wavulana (4) wa kijiji wapo kijiweni wamekaa kwenye gogo wakiwa wamezunguukwa na miti wakijadili kwenda kuiba shambani.
Mvulana mmoja: JUMA
Anasimama kisha anaongea.
Sikilizeni kwanza inabidi tujadili shamba gani tunaenda.
Mvulana wa pili: OTHU
Akimwangalia Juma usoni.
Mashamba yapo mengi tuchague! Sio kitu cha kujadili!
Mvulana wa tatu: RAMSO
Kwanza leo tuende shamba la yule mama Salome.
Mvulana wa nne: JOSE
Akishtuka na kutoa macho.
Mmenikumbusha, mna muonaje yule mtoto Salome?
OTHU
Akimwangalia Jose kwa mshangao.
Kafanya nini?
JOSE
Mimi namtaka tusaidiane kumpata, halafu kama kawaida tunashilikiana.
RAMSO
Akiongea kwa dharau.
Acheni kujipa tabu yule, tunamkamata tunambaka!
OTHU
Akimwangalia Ramso kwa furaha.
Halafu nimekumbuka wale wanakuwaga Salome na wenzake.
JOSE
Akiinuka na kuongea.
Twendeni kwenye hilo shamba! Kuhusu Salome na rafiki zake tunamkamata mmoja mmoja, tunambaka! Hakuna kumbembeleza! Sisi ndio watoto wa kijijini!
JUMA
Anainuka huku anacheka.
Hilo ndio la maana Jose! Twendeni shamba, mimi njaa inauma kuhusu hao watoto tutawakamata tu mmoja mmoja.
SINI: 7
MCHANA SAA 8
Salome akiwa na marafiki zake watatu Mariamu, Happy na Jane wanaruka kamba uwanjani mbali kidogo na nyumbani kwao. Mara Othu, Ramso, Juma, Jose wanapita wanawaona wakina Salome wanacheza kamba. Salome anarusha yeye na Jeni. Mariamu anaruka. Mara Ramso na rafiki zake wanafika karibu na wakina Salome.
JUMA
Akiongea kwa ukali!
We Mariamu hebu njoo mwenyewe!
RAMSO
Akiongea kwa dharau.
Hakuna kumbembeleza mtu!
SALOME
Anaachia kamba na kumwangalia Ramso.
Hivi nyinyi kwanini hamna ustaarabu?
JOSE
Akimnyoshea kidole cha shahada.
Tena wewe nyamaza zamu yako bado.
SALOME
Akishangaa na kukunja sura.
Zamu ya nini?
JENI
Akishanga na kukunja kamba.
Jamani si mnawajua hao walivyo wakorofi. Bora tuondoke maana wana sifa kama nguru.
RAMSO
Akicheka kwa dharau huku akiwaangalia.
Eti mwondoke! Haondoki mtu. Leo ndo leo!
KATI KUBWA
Salome na wenzake wanaonekana wakikimbia huku. Wakina Ramso wanawakimbiza. Mara Salome anapotezana na wenzake. Salome anakimbilia porini. Anapogeuka nyuma anawaona Ramso na wenzake wanakuja. Anaamua kukimbilia nyuma ya mti mkubwa kwa kujificha.
Ramso na wenzake wanasimama kwenye huo mti aliojificha Salome. Salome anatetemeka kwa uwoga na kuamua kutokambio. Ramso na wenzake wanasikia kishindo cha Salome. Anapokimbia na kufika mbali kidogo anachoka sana. Mara anapumzika na anakamatwa na wakina Ramso.
JUMA
Anaongea huku akihema akiwa na hasira macho kayatoa.
Yaani wewe unaweza vipi kutusumbua sisi?
SALOME
Akiwa na uwoga huku akihema.
Kwani nimewafanyia nini na mnataka nini kwangu?
RAMSO
Akimwangalia Juma na Othu.
Jamani mshikeni! Nianze mimi.
Juma na Othu wanamshika Salome.
SALOME
Akitoa macho kwa mshangao huku akitetemeka na machozi yakimtoka.
Jamani ndio mnataka kunibaka nioneeni huruma mnanipotezea ndoto zangu za baadaye!
Akilia.
RAMSO
Anaongea kwa dharau huku akimwangalia Salome.
Ahaha! Na mimi hii ndio ndoto yangu!
Mara wababa wazima wanatokea wakiwa wamebeba kuni. Ramso na wenzake wanakimbia wakiwa hawajambaka Salome anainuliwa na wale wababa wanampeleka kwao. Salome huku akibubujikwa na machozi kwa uchungu.
KATI KUBWA
Wale wababa na Salome wanaonekana kwa kina Salome. Wamekaa chini na mama Salome na baba Salome. Salome anahadithia yaliomkuta mpaka kuletwa na wale wababa.
MAMA SALOME
Akishangaa kwa kelele huku akinyanyuka.
Ehe!, ehe!, ehe! Sikubali hata kama bado hawajambaka mwanangu kuwaachia hawa vijana watazoea. Nimesema sikubali!
SALOME
Anaonekana akibubujika machozi huku akiinamia chini.
BABA SALOME
Anaonekana akinyanyuka na kuongea huku anaondoka na kuelekea kwa kina Ramso.
Sasa wamechokoza moto wao siwanajifanya hawasikii hapa kijijini leowataniona.
WABABA 2
Wana nyanyuka na kumuaga Salome na mama yake.
Sisi tunaenda. Pole Salome.
SALOME
Akiwaangalia huku akilia kisha anaitikia na kichwa.
WABABA 2
Wananyanyua kuni zao na kumwangalia mama Salome.
Mama Salome, tuweni waangalifu na hawa vijana. Sisi tunaenda.
MAMA SALOME
Akimuinua Salome huku akiongea.
Haya karibuni, lakini lazima niwafundishe adabu…
SINI: 8
SIKU NYINGINE
Baba Salome na mama Salome na wazazi wa Ramso wanaonekana wakikaa kwa kina Ramso wamekaa kwenye mkeka wakiongea.
BABA SALOME
Akiongea kwa hasira.
Najua mnajua kitendo alichokifanya mwanenu.
MAMA RAMSO
Akishusha pumzi na kuongea.
Ndio jana tumesikia hata sisi tumesikitika na hata hivyo Ramso na wenzake. Mpaka leo hawaonekani.
MAMA SALOME
Akiongea kwa hasira huku akimwangalia mama Ramso.
Nyinyi mmepanga kuwatorosha. Lakini sawa!
MAMA SALOME
Akiongea kwa uzuni.
Sio hivyo mama Salome. Mimi na wewe tuna uchungu kama wanawake. Na kama mtoto angekuwa nguo ningegawa.
BABA RAMSO
Kweli Ramso angekuwa nguo tungekuwa hatunaye zamani.
MAMA RAMSO
Sisi tunachoomba mtusamee sisi. Na hata kama tukimuona tutamkamata kama sio yeye yoyote kati yao tutampeleka serikali ya kijiji. Tena sisi tupo pamoja na nyinyi.
BABA SALOME
Ananyanyuka na kumshika mkono mke wake.
Mke wangu, tuondoke.
SINI: 9
JIONI
Ramso na wenzake wanaonekana wakijadiliana wakiwa kichakani.
JUMA
Akiwangalia Othu pamoja na Ramso.
Jamani sasa itakuwaje?
OTHU
Kakaa chini kajinamia huku akivunjavunja vijiti.
Yaani mimi mwenyewe sielewi.
RAMSO
Akiongea huku kasimama.
Sio swala la kujadiliana kilichobaki ni kwenda kijiji kingine kwenda kuanza maisha mapya.
OTHU
Anainuka chini huku akijikung’uta majani.
Hilo wazo zuri maana…
WOTE
Wanaonekana wanaondoka. Gafla wanakutana na baba Salome. Wanajificha kwenye mti. Baba Salome anapita katika mti huo akiwa amebeba jembe begani. Anaelekea nyumbani kwake. Ramso na wenzake wanatoka mbio wakiwa wanarukaruka mashamba ya watu.
SINI: 10
Salome na wenzake Jeni na Mariamu wakiwa kisimani wanateka maji huku wakiwa wanajadili vitendo vya kina Ramso.
JENI
Akinyanyua ndoo akiweka pembeni huku akiwa anaongea.
Afadhali walivyokukosa maana wangekufanyia kitendo cha aibu…
SALOME
Akiweka kata kwenye ndoo yake.
Jamani acheni mungu aitwe mungu. Siamini kama nimenusurika...
MARIAMU
Akimwangalia Salome.
Inabidi uamini kama umenusurika na umshukuru mungu kwa kuwaleta wale wababa!
JENI
Akimwangalia Mariamu.
Unachoongea Mariamu ni kweli inatakiwa umshukuru sana mungu.
SALOME
Akiweka kata chini anasimama na kushika kiuno.
Nyie acheni tu tubebeni ndoo tuondokeni.
KATI KUBWA
Salome na wenzake wanaonekana wanabeba ndoo wanaondoka. Mara Salome anafika kwao anatua ndoo huku mama yake akipepea moto.
SINI: 11
USIKU
Salome anaonekana akiwa chumbani kwake. Anawaza hatari iliyotaka kumkuta. Mara mama yake anaingia chumbani kwake.
MAMA SALOME
Hivi kibiriti kiko wapi?
SALOME
Anastuka na kujifuta machozi.
Kipo… kipo… jikoni.
MAMA SALOME
Akikaa kitandani kwa Salome na kuongea nae akimwangalia usoni.
Ina maana bado tu haujasahau hayo mambo tushayashughulikia. Si unajua watu wenyewe wamekimbia.
SALOME
Ndio na jua mama, ila nasikia uchungu kijijini kote wanaadithia habari zangu.
MAMA SALOME
Anamfuta machozi Salome.
Aaah! We waache tu waongee we lala!
Ananyanyuka na kuelekea chumbani kwake.
SALOME
Anazima kibatari. Analala na kujifunika kanga.
SINI: 12
Ramso na wenzake wanaonekana wakiwa wamekaa sehemu huku wanajadiliana.
JUMA
Jamani nimepata wazo. Twendeni kwa mganaga. Hali hii mpaka lini?
OTHU
Eheeee hilo wazo zuri. Na mimi nimeshachoka kukimbiakimbia.
RAMSO
Akimwangalia usoni Juma.
Sasa huko kwa mganga tunaenda kufanya nini?
JUMA
Anaonekana akimwangalia Othu usoni na Ramso.
Ina maana nyie hamujui tunaenda kufanya nini kwa mganga.
OTHU
Anaonekana nae na shauku ya kutaka kujua.
Ndio hata mimi nimemuunga mkono kuwa wazo lako zuri. Pia hata mimi sijui nitanaenda kufanya nini. Na ni dawa aina gani? Nimesapoti kuona wazo zuri sababu tu nimechoka maisha ya kukimbiakimbia
JUMA
Akiwa anaongea kwa kujiamini.
Kwanza kabisa tupate dawa la kuwashaurisha wana kijiji makosa tuliyo yafanya pili tukienda kuiba hawatuoni. Au nyie mnaonaje?
OTHU
Kweli jamani tuondokeni tukamtafute huyo mganga!
SINI: 13
Baba Salome anaenda kijiji cha tatu kwenda kusalimia kwa baba yake na mama yake. Wanaonekana wamekaa chini ya muembe wakijidaliana kuhusu Salome akeketwe.
BIBI
Akiongea huku akimwangalia baba Salome usoni.
Hivi binti yakoa tafanyiwa lini tohara maana umri unaenda
BABA SALOME
Yaani mama hili swala sijui hata litakuwaje?
BABU
Anainuka na kuongea kwa hasira.
Nimesema mwezi wa kumi na mbili nakuja na mama yako kumfanyia mila.
BIBI
Anainuka nakuongea kwa hasira.
Heee! Ukaongee na mke wako mwezi wa kumi na mbili ndio hivyo hatutaki aibu! Anaelekea ndani.
KATI KUBWA
Baba Salome na babu Salome wanaonekana wanatoka shamba na majembe yakiwa begani. Huku bibi Salome akiwaelekeza wakina Ramso kwa mganga. Mara baba Salome na babu Salome wanashikana kutua majembe kisha baba Salome anachukuwa ndoo na kuelekea kisimani. Anaelekea njia ile ile wanaopita wakina Ramso.
BABU SALOME
Akiangalia mlango huku akimwita bibi Salome.
Bibi Salome, hebu njoo umuangalie baba Salome.
BIBI SALOME
Anatoka nje kwa mshangao.
Kafanyaje!
BABU SALOME
Akimnyoshea kidole baba Salome.
Yule mwangalie! Karudi shambani sasa hivi na anaelekea kisimani.
BIBI SALOME
Akiachia mdomo kwa mshangao.
He!
Akimwita baba Salome.
We baba Salome…
BABA SALOME
Anaonekana akigeuka nyuma.
BIBI SALOME
Akiongea kwa sauti ya juu.
Hebu rudi! Kwa nini unajitesa kama hivyo?
BABU SALOME
Anaonekana akitandika mkeka na kulala.
BABA SALOME
Anaonekana akiweka ndoo chini na kuongea na bibi Salome.
Unasemaje mama?
BIBI SALOME
Kesho asubuhi unaondoka acha kujichosha! Hebu nenda kapumzike na baba yako yupo pale kwenye mkeka.
Kisha anaingia ndani.
BABA SALOME
Anaonekana akielekea kwenye mkeka huku akitabasamu na kuongea peke yake.
Kweli uchungu wa mwana ajuwae mazazi.
SINI: 15
Baba Salome na mama Salome wakiwa wanakula huku Salome akiwa anaongelea kuhusu mtihani wa taifa.
SALOME
Salome akimwangalia baba yake na mama yake huku akiwa kashika chakula mikononi na kuanza kuongea kwa furaha.
Na wahaidi wazazi wangu ni lazima ni fahulu ili shida zituishe.
MAMA SALOME
Akimwangalia Salome.
Aliekuambia ukifaulu shida ndo zinaisha. Yani kusoma ni kutoa ujinga.
BABA SALOME
Baada ya kuzungumza mambo ya maana wakati kesho shamba. Mbona mtoto wa mzee karinga kasomaa lakini bado anakata mkaa?
SALOME
Lakini baba…
kwa unyonge.
MAMA SALOME
Sio lakini! Lakini jitahidi ufike chuo. Kuna vitu vingi unatakiwa ujiepushe navyo.
BABA SALOME
Anaonekana akinawa mikono huku sura inaonekana ajapendezewa na maongezi yale.
SINI: 16
USIKU
Baba Salome na mama Salome wanaonekana wakiwa chumbani wakiwa wanabishana kuhusu Salome kukeketwa.
MAMA SALOME
Akiongea kwa hasira na sauti ya juu.
Nimesema mwanangu hafanyiwi tohara.
BABA SALOME
Akiongea kwa hasira.
Humu ndani nani mwanaume na ni nani baba wa Salome?
MAMA SALOME
Hata kama mnataka kuniulia mwanangu.
SALOME
Akiwa chumbani kwake tayari kulala. Anasikia mabishano kwa mbali lakini haelewi kinacho endelea anaamua kugeukia upande wa pili wa kitanda na kuendelea kulala.
BABA SALOME
Akiongea sauti ya juu yenye hasira.
Mimi ndio nimeshasema baba na mama nishaongea nao na mila yetu ina sema ivyo Salome lazima afanyiwe tohara.
MAMA SALOME
Lakini baba Salome si unaelewa athali zakukeketwa?
BABA SALOME
Akiongea kwa hasira.
We nyamaza. Nisije kukupiga sasa hivi.
MAMA SALOME
Akiwa kachukia huku akimwangalia baba Salome.
Unipige kwa lipi kukwambia ukweli ndo unipige eh!
SINI: 17
ASUBUHI
Salome akiwa anaondoka kuelekea shule. Mama Salome anaonekana akimwangalia Salome kwa huruma kwa kitendo anachotaka kufanyiwa huku akiwa anasisitiza kwa kutingisha kichwa.
KATI KUBWA
Wanaonekana Juma, Ramso na Othu wakiwa kwa mganga. Anaonekana akiwapokea huku akiimba nyimbo zake za mizimu ya kolelo.
MGANGA
Mganga anaimba huku akiwakaribisha wakina Ramso.
Mnaonekana mna matatizo makubwa sana.
RAMSO NA WENZAKE
Wakitetemeka kwa hofu. Wakijibu kwa pamoja.
Ndio mganga tuna matatizo.
MGANGA
Akiongea kwa sauti ya juu huku akitoa macho.
Semeni shida yenu!
JUMA
Akiongea kwa hofu.
Salome, mganga.
MGANGA
Akicheka kwa sauti ya juu kisha anaongea.
Salome… Salome… Salome…
OTHU
Ndio mganga Salome! Tunatafutwa kwa ajili yake tunataka dawa la kusahau katika kijiji kizima.
MGANGA
Poleni sana! Maana kijiji kizima kimepanga kuwafanyia kitu kibaya. Sasa kwanza wekeni hela zenu katika chungu kisha nawapatia dawa ya kuwasaurisha kabisa makosa yenu kwenye kijiji. Pili nataka muniambie nyinyi katika kijiji chenu mnafanya kazi gani na msinifiche na mkinificha dawa itakataa kufanya kazi!
JUMA
Akiongea kwa wasiwasi mkubwa.
Mganga sisi kazi yetu kuibaiba mashambani, ndizi, miogo, mahindi kisha tunaenda kuuza.
MGANGA
Ehee! Sasa hivi dawa nitayowapa itawasaidia mkienda kuiba hawawaoni kabisa hata mkipita mbele yao.
JUMA NA WENZAKE
Wakiwa wenye sura za furaha kupata dawa waliongea pamaoja.
Asante sana mganga.
Huku wanaondoka.
MGANGA
Baada ya wakina Juma kuondoka, mganga alianza kucheka na kuona wajinga wakina Ramso huku akiongea na msaidizi wake.
Wale watoto wajinga nimewapa dawa za uwongo. Waache wakakamatwe ili wajifunze.
SINI: 18
ASUBUHI
BABA SALOME
Anaonekana kavua shati kapachika begani. Anatoka nje kibarazani kwake kisha anamuita mama Salome akiwa anaosha vyombo.
Mama Salome njoo mara moja chumbani nina maongezi na wewe!
MAMA SALOME
Eeh!? Nini tena mume wangu?
Huku ananyanyuka nakuelekea chumbani.
BABA SALOME
Anaonekana akiwa siriasi kupita kawaida.
Mke wangu, naona unanipanda kichwani na nataka leo hii tukubaliane kuhusu Salome kukeketwa. Mama yangu nitamueleza nini baba pia mila zetu na hata mizimu ya ukoo wetu na isitoshe familia yetu wote wamekeketwa sasa. Tukimuacha Salome sisi tutachekwa na wanakijiji wote najaribu kufikiria kwa kina mke wangu.
MAMA SALOME
Anaonekana akiwa kanyamaza kimya huku akiwa anaguna.
mmh!...
BABA SALOME
Anaonekana akiwa anamwangalia kwa hasira mama Salome.
Sasa unamaanisha nini ukinyamaza kimya?
MAMA SALOME
Akiwa anaongea kwa unyonge.
Baba Salome! Salome mwenyewe leo ndio kaenda kufanya mtihani wa taifa kumaliza darasa la saba. Sisi huku nyumbani tunagombana. We huoni tutasababisha afeli mtihani.
BABA SALOME
Akiwa anaonesha ukali wa maneno akipaza sauti.
Sasa uko pamoja na mimi au laa?
MAMA SALOME
Akionekana kususa huku akitoka chumbani kuelekea nje.
Bwana fanya tu unavyojua…
SINI: 19
BAADA YA MIEZI 2
Salome na wenzake wanaonekana wakiwa wanaangalia majibu ya mtihani wa taifa. Salome huku akijikuta amefaulu kipaji mjini kisha anaelekea nyumbani akiwa mwenye furaha kuwaeleza wazazi wake.
SINI: 20
SALOME
Akiwa mwenye furaha anaongea na mama yake.
Mama nimefahulu! Tena shule ya kipaji mjini!
MAMA SALOME
Akimuuliza kwa unyonge.
Kweli mwanangu hongera!
SALOME
Akimwangalia mama yake.
Mama mbona hauna furaha? Unaumwa? Halafu baba yuko wapi nae nimwambie!
MAMA SALOME
Akiwa bado mnyonge
Hapana mwanangu niko sawa. Siumwi. Baba yako kaenda kijiji cha pili kwenda kumchukua babu yako na bibi yako watakuja kesho asubuhi. Tena utawaambia wote kwa pamoja.
SALOME
He jamani! Baba safari hii hajaniaga dah!
SINI: 21
BABU
Akiwa anawaangalia wote.
Jamani ayawi ayawi sasa yamekuwa! Hebu bibi Salome tueleze umefikia wapi ili Salome awekwe ndani. Maana swala hili limeshafika wakati wake linatakiwa lifanyike haraka.
BIBI SALOME
Akiwa anajihami na kuongea huku akionyesha furaha.
Mimi nimeshaongea na Ngariba. Kesho asubui watakuwa wameshafika.
MAMA SALOME
Akionyesha mwenye hofu.
Sitoamini mpaka mwanangu nione yuko salama ndo kweli nitaona nimekuza!
BABA SALOME
Akicheka kwa sauti.
Ahahahaaaa!! Mpaka hapa tumekuza inabidi tukamchukuwe Salome tumuweke ndani.
SALOME
Wakati wakifanya majadiliano hayo, Salome alikuwa dirishani kajificha. Anasikiliza wanachoongea.
BIBI SALOME
Asije akachoka leo wakati kesho mama mwali unatakiwa apumzike. Twende nikausaidie kuongea na Salome ili akae ndani maana watoto wa siku hizi anaweza akakuchosha bure.
Anainuka na mama Salome huku wanacheka.
KATI KUBWA
Mama Salome na bibi Salome wanapofika jikoni wanakuta chakula kinaungua na Salome hayupo. Wanaita bila mafanikio. Wanaenda kuwataarifu baba Salome na babu yake Salome kuwaeleza kuwa Salome haonekani. Baba na babu wanashtuka.
MAMA SALOME
Akiongea kwa wasiwasi.
Jamani Salome haonekani na kaacha chakula kinaungua.
BABU SALOME
Akistuka.
Kwa nini anaondoka na kuacha chakula kinaungua na hiyo tabia gani?
BABA SALOME
Anaonekana akifikiria kitu huku anaongea.
Jamani Salome! Mbona hajawahi kufanya kitu cha ajabu kama hiki?
MAMA SALOME
Anaonekana kama kachanganyikiwa.
Lakini kweli baba Salome, atakuwa kaenda wapi? Kila akitoka lazima aage.
BABU SALOME
Basi kama ndo hivyo tusifanye masiala. Inabidi akatafutwe.
SALOME
(Nyimbo inasindikiza kilio.)
Anaonekana akikimbia huku akilia na kuelekea porini. Anapofika katikati ya pori anakaa chini na kuanza kulia kwa uchungu huku akiongea.
Mimi sikubali, sirudi nyumbani mpaka wasahau ni bora niepushe uwahi wangu kwa kukaa huku kwa muda.
Akiendelea kulia kwa uchungu.
(Nyimbo ya Salome inasindikiza kilio.)
KATI KUBWA
Mama Salome, baba Salome, babu Salome, pamoja na bibi Salome wanaulizia kila nyumba za marafiki zake bila ya mafanikio. Wanaonekana kuchanganyikiwa na kuelekea kwenye maeneo mengine kumtafuta.
MAMA SALOME
Akiwa kachanganyikiwa na kuongea akiwa na uchungu.
Sasa mwanangu atakuwa kaelekea wapi au atakuwakachukuliwa na nani, hajawahi kuondoka bila kuaga.
BIBI SALOME
Akimuangalia mama Salome.
Sasa mwanangu usilalamike twende tukamtafute.
MAMA SALOME
Sasa mama mpaka saa hizi saa kumi na moja hatujamuona.
BABA SALOME
Akiongea kwa jazba kidogo.
Tunaangaika hivi halafu asije. Akawa katoroshwa na mwanaume.
BIBI SALOME
Mmmmh!! Hayo yanawezekana. Watoto wa siku hizi.
BABA SALOME
Kuwa nimekumbuka sisumbuki kumtafuta. Haiwezekani mtu aondoke gafla huyu kashaondoka na mwanaume!
BABU SALOME
Akimwangalia baba Salome kwa unyonge.
Usiseme hivo sasa huyu mzazi mwenzako si una mvunja nguvu.
BABA SALOME
Sio hivo baba.
Wakiendelea kutembea kumtafuta.
KATI KUBWA
Wakiwa wanaendelea kumtafuta walipofika katikati ya pori wanashtuka.
Wanapoona kichwa cha Salome na chini kuna damu nyingi na wote wanaishiwa na nguvu na mama Salome anazimia.
Itaendelea part two…
Story
Oliver John
CAST
1) Baba Salome
2) Mama Salome
3) Babu Salome
4) Bibi Salome
5) Salome
6) Ramso
7) Baba ramso
8) Mama ramso
9) Juma
10) Jose
11) Othu
12) Mganga
13) Mbaba namba:1
14) Mbaba namba:2
15) Maliamu
16) Happy
17) Jeni
18) Mwanafunzi 1
19) Mwanafunzi 2
20) Wa baba
wawili
STORY
OLIVER JOHN
SCRIPT WRITER
AISHA ATHUMANI
SCRIPT EDITING
ERICK GABRIELY
FRANZISKA MUELLER
DIRECTOR
_______________________
ASSISTANCE DIRECTOR
_________________________________
PRODUCED BY
_______________________________
MAKE UP
____________________________________
CASTING DIRCTOR
______________________________
You can do it, too! Sign up for free now at https://www.jimdo.com