Amka! ni albamu yangu ya kwanza ambayo kwa sasa iko sokoni. Albamu hii imetungwa na kupigwa kwa vionjo vya asili ya makabila yetu ya hapa Tanzania. Vionjo hivi ambavyo ni marimba, ngoma, manyanga, filimbi na kuimba kwa kuchanganya makabila. Pia naendelea katika utafiti kwa kutafuta muziki halisi wa Tanzania.
Mpaka sasa zimetoka nyimbo nane za audio na video tatu ambazo unaweza kuziangalia na kusikiliza hapo chini. Maandishi yake yote unasoma ukibonyeza hapo.
Ukitaka kununua albamu ya audio au albamu ya video bonyeza hapo na tafuta mawasiliano na mimi.
Pachingo Mbaride maana yake kigeugeu, nazungumzia mtu ambaye anapenda kulalamika na kuamini imani za ushirikina kumbe yeye mwenyewe ndiye anakosea mwenendo wa maisha yake nakupeleka lawama kwa majirani zake kuwa wanamroga isipokuwa yeye mwenyewe ndiye anajiroga. Kwa kusoma maandishi yake bonyeza hapo.
Nyimbo hii ya Amka inazungumzia utu wetu na utamaduni wetu na vivutio tulivyo navyo Tanzania. Kwa kusoma maadishi yake bonyeza hapo.
Nazungumzia hali halisi ya mapenzi. Kwa kusoma maadishi yake bonyeza hapa.
Hii Video itafuata badaye. Kusoma maandishi yake sasa hivi bonyeza hapa.
You can do it, too! Sign up for free now at https://www.jimdo.com